top of page

MOHAMED ISMAT MOHAMED

Mombasa, KENYA

Picha: Samia Salim
IMG-5974.JPG
Picha: Omar Banafa

"Wewe ni wa kipekee. Una talanta na uwezo tofauti. Hauhitaji daima kufuata nyayo za wengine."

MOHAMED ISMAT MOHAMED (Mombasa, Kenya)

MOHAMED ISMAT MOHAMED (Mombasa, Kenya)

Play Video
Muziki: Siku nyepesi na Sauti Sol (instrumental ft. Soweto gospel choir)

"Nilikuwa katika shule ya Waislam kama kawaida, nikikaa ambapo kila wakati huwa karibu na Dirisha  kuhisi kupendeza kwa hewa wakati niliposoma Quran kwa sauti ya chini.  Ghafla,  nilihisi fimbo ikigonga nyuma ya kichwa changu kwa jicho  la kushoto na mwalimu wangu.  Nilienda tu nyumbani, Huku jicho langu likihisi uchungu kidogo mwanzoni.  Lakini niliona hakuna tatizo lolote lililotokeaa. 

 

Mama yangu alijaribu kutumia dawa fulani za kinyumbani, lakini haikufaulu.  Daktari alisema "Hautaweza kuona tena kwa jicho lako la kushoto".  Katika wakati huo, sauti yake ilikuwa sauti laini kabisa , wak"

IMG-5977.JPG
IMG-6064.JPG
Picha: Omar Banafa
Picha: Omar Banafa
Picha: Omar Banafa
Mohamed Ismat Mohamed's S.C.A.R.S. Story (Mombasa, Kenya)

Mohamed Ismat Mohamed's S.C.A.R.S. Story (Mombasa, Kenya)

Play Video

Kucheza ni maisha

Haikua rahisi kujikubali katika hali nilionayo sasa

Kwa kupoteza jicho langu bila matarajio kuwa sitaeza kuona kabisa maishani mwangu.

Kamwe sikuchoka kufanya kile ninachopenda kwenye densi,

Sarakasi na hata nilianza kuwapa motisha, Kufunza wale waliopata majeraha na kufa moyo katika kutafuta riziki zao kwa njia moja au nyingine.

Pindi tu ninapopatana nao huwaacha na msemo huu

Katika kila jambo lilotokea Mungu ako na sababu zake.

Ati mapigo ya moyo wangu ndio sauti kubwa kabisa ambayo nimewahi kusikia.

Mohamed Ismat Mohamed alizaliwa Mombasa, Kenya na alikulia pwani. Katika maisha yake yote, amekuwa katika sanaa. Alianza kufundisha densi mnamo 2013 na tangu siku hiyo, maisha yake yamekuwa kwenye talanta ikiwemo sarakasi,densi na amepata nafasi za kusafiri ndani ya nchi na nje kuonyesha ujuzi wake.

 

Alihamia katika mji mkuu wa Nairobi mnamo Oktoba 2014, ili kutafuta matarajio mazuri na yenye manufaa zaidi . Mnamo mwaka wa 2016 Alianza mradi na rafiki yake mmoja inayoitwa "Kuja kwenye kijiji chako" ambapo wanafundisha Densi kwa jamii. Alianzisha "Kikao cha Densi", katika kijiji chake cha Mombasa. Hii iliwatia moyo wanafunzi wake kujifunza na kutambua asili ya muziki na mtindo wa densi. Aliunda kikundi cha vijana, ambacho mwishowe ikawa kampuni ya densi.

 

Alianza kusoma yoga na akapata uthibitisho wa kufundisha mnamo 2017. Wakati wa mchakato wake wa uponyaji yoga ilitumika kama zana nzuri ya kuondokana na mafadhaiko wakati wengine wangemdhihaki au kuhisi kukosa kutosha kwa kuwa tofauti. Mohamed amefundisha kitaifa huko Mombasa, Nairobi, Malindi na Voi . Anaendelea kuandaa semina za densi na yoga kwa wanaoinukia sasa kwenye hii sanaa.

 

Mohamed hupata shauku kubwa katika kufundisha densi, yoga na sarakasi. Anathamani fursa za kushiriki ujuzi wake na maarifa kwa wengine, wakati pia hubadilishana mawazo na kujifunza vitu tofauti . Hajihisi tu kuvunjika nguvu kwa kutokukata tamaa na kuendelea kufanya kile anapenda licha ya hadithi yake . Uzoefu wake pia umemruhusu kuungana kwa undani zaidi na marafiki, familia na wenzake.

bottom of page